BREAKING NEWSSSS: MSANII YP WA TMK WANAUME FAMILY AFARIKI DUNIA

Msanii 'YP' toka kundi la TMK Wanaume Family amefariki dunia jana usiku katika hospitali ya Temeke ambako alikuwa akipatiwa matibabu akisumbiliwa na kifua kwa muda mrefu lakini hali ilikuwa mbaya katika wiki mbili kabla ya kifo chake.

Meneja wa TMK Wanaume Family Said Fela amethibitisha kutokea kwa msiba huo. Msiba wa msanii huyo uko Keko nyumbani kwa baba yake.

Said Fella amesema Marehemu ambaye jina lake halisi ni Yessaya Ambikile alifanya vizuri na msanii mwingine Y Dash na nyimbo kama 'Ulipenda Pesa', 'Pumzika', 'Shemsha' na nyimbo nyingi za TMK Wanaume Family kama 'Twende zetu' ya Chege, 'Dar mpaka Moro', 'Kichwa kinauma', 'Tufurahi' na nyimbo nyingi za TMK Wanaume family.

Anna Peter Fredz
R.I.P YP

ANGALIA VIDEO HII YA KICHWA KINAUMA AMBAPO NA YEYE ALISHIRIKI


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo