WANANCHI WAHIMIZWA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

WANANCHI wa Wilaya ya Butiama mkoani Mara, wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupiga kura ili uchaguzi utakapofika waweze kupata haki yao ya msingi ya  kuwachagua viongozi wanaowataka.

Kauli hiyo imetolewa na mjumbe wa Kamati Tendaji ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilaya ya Butiama, Yusufu Kazi, wakati akiwashukuru wajumbe kwa kumuamini na kumpa kura nyingi kwenye uchaguzi wa mkutano mkuu wa Jimbo uliofanyika hivi karibuni.

Kazi, alisema wananchi wote wanatakiwa kwenda kujiandikisha kwenye daftari hilo zoezi litakapoanza, kwani bila kujiandikisha watakosa haki yao ya msingi ya kuwachagua viongozi wanaowataka kwa ajili ya maendeleo yao.

Pamoja na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari hilo, alitoa shukrani kwa Rais Jakaya Kikwete kwa kuwapa Wilaya Butiama.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo