Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakimpa kichapo mwandishi wa
habari wa gazeti la Tanzania Daima, Josephat Isango, nje ya Makao Makuu
ya Polisi, Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika akizungumza na waandishi wa
habari waliokuwepo kwenye eneo la makao makuu ya Jeshi la Polisi,juu ya
kile kilichokuwa kikiendelea kwenye mahojiani katika ya Mwenyekiti wa
Chama hicho na Jeshi la Polisi.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe
akiwasili kwenye makao makuu ya Jeshi la Polisi nchini,Mapema JANA
asubuhi tayari kwa kwenda kuhojiwa juu kauli aliyoitoa kwenye Mkutano
Mkuu wa chama hicho hivi katibuni,kuwa watafanya maandamano nchini nzima
bila kikomo.
Makamu Mwenyekiti wa Chadema,Prof. Abdallah Safari na Wakili wa
Chama,Wakili Mabele Marando wakiwasili kwenye Makao Makuu wa Jeshi la
Polisi mapema JANA.
Baadhi ya Wachama na Wafuafi wa Chadema wakishangilia wakati Mwenyekiti wao akiwasili kwenye Makao Makuu ya Jeshi la Palisi.
Ulinzi mlali katika eneo hilo.
Askari akiwataka wanachadema kuondoka.
Huyu alikuwa akikaidi amri ya Jeshi la Polisi ilibidi aondolewe kwa nguvu.
Mmoja wa wanachama wa CHADEMA mbaye jina lake halikuweza kupatikana,
akipewa kibano na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), nje ya
Makao Makuu ya Polisi, Dar es Salaam.
Ulinzi mkali.
Mwenyekiti wa Chama cha DP, Christopher Mtikila akihojiwa na askari
Polisi, alipowasili Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam kwa
kutumia usafiri wa bajaji, ambako Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe
alihojiwa na Polisi.
