Katika hali isiyotarajiwa, mwanafunzi wa Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Ezra Gerald (19), amejinyonga hadi kufa kwa kutumia shuka ya hospitali, alikokuwa amelazwa kwa kile kinachoeleza alikuwa anasumbuliwa na homa ya matumbo.
Hata
hivyo, ujumbe ulioachwa na marehemu huyo unaonesha alichukua uamuzi
huo, kutokana na kuchukizwa na uamuzi wa daktari aliyemhudumia wa
kumlaza ili atibiwe ugonjwa ambao hakuwa anaumwa.
Aidha, katika ujumbe huo imeelezwa alichukizwa na kitendo cha kupotezewa muda hospitalini wakati wenzake wakiendelea na masomo.
Tukio
hilo limethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Gilles
Muroto aliyesema mwanafunzi huo alijinyonga Septemba 16 mwaka huu saa
moja asubuhi.
Alisema
mwili wake uligundulika ukining’inia kwenye mti uliopo maeneo ya
hospitali hiyo na alipopekuliwa katika mifuko ya suruali yake,
zilionekana karatasi mbili, moja ikiwa na ujumbe uliosomeka; “Haiwezekani
binadamu kuhudumiwa kama mbwa, yaani nafika hospitali najieleza hali
yangu halafu daktari ananiandikia kulazwa bila kupima, sasa sijui
wanatibu nini?
“Kwa
kweli siwezi kuvumilia wenzangu wanasoma halafu mimi nimekalishwa tu
hapa hospitali bila kujua wananitibu nini, inaniuma sana mpaka nafikia
hatua hii ya kujiondoa duniani kwa sababu naona watu wanachezea ndoto
zangu, mimi siwezi kuona ndoto yangu inazimwa wakati natakiwa niwepo
shuleni nikamilishe ndoto zangu “mjitahidi tukutane mbinguni “Respect My
Family and Brother Henry.”
Kamanda Muroto amesema hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo, lakini polisi wanaendelea na uchunguzi.
Inaelezwa mwanafunzi huyo aliyetajwa kuwa ni mwenyeji wa mkoa wa Tabora, alilazwa hospitalini hapo tangu Septemba 11 mwaka huu.
Kwa
mujibu wa Katibu wa Hospitali ya Mkoa wa Kagera, Benges Justus, tukio
hilo lilitokea Septemba 16, mwaka huu, siku moja baada ya mgonjwa huyo
kulazwa.
Alisema
baada ya mwanafunzi huyo kupokelewa hospitalini hapo, alifanyiwa vipimo
vyote vya kitabibu na kugundulika anasumbuliwa na malaria, ndipo
akaanzishiwa tiba ya ugonjwa huo.
