MTIHANI WA DARASA LA SABA 2014 WILAYANI MAKETE WAMALIZIKA KWA AMANI NA UTULIVU

Zaidi ya wanafunzi 2,178  wamemaliza  mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi  wilayani Makete mkoani Njombe katika hali ya utulivu na amani 

Mitihani hiyo iliyoanza hapo jana katika shule zote za msingi nchini  kwa zaidi ya wanafunzi 808,11 kuanza mitihani hiyo nchi nzima huku katika wilaya ya Makete wanafunzi walio fanya mtihani ni 2,178  wavulana wakiwa 1,045 na wasichana wakiwa 1,133  na wamemaliza hii leo bila kuripotiwa vitendo vya udanganyifu wala dosari   

Idadi hiyo ni tofauti na mwaka uliopita ambapo zaidi ya wahitimu 844,938 walifanya mtihani huo nchi nzima

Eddy blog imetembelea katika vituo vya mtihani na kushudia hali ya utulivu na wanafunzi wakiwa katika vyumba vya mtihani huku ulinzi ukionekana kuimarishwa jambo ambalo limesaidia mtihani hiyo kuendelea kufanyika hadi mwisho bila matatizo

Kwa upande wao wazazi na walezi  wamepongeza idara ya elimu kwa kusimamia mitihani hiyo na kuomba  walimu wanaopewa dhamana ya kusimamia wawe wazalendo kwa kuto jihusisha na udanganyifu  wakati wa mitihani hiyo katika kipindi kijacho

Mapema wiki hii Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenister Mhagama alizitaka kamati za mtihani mikoa na wilaya kusimamia ipasavyo kuepuka vitendo vitakavyopelekea mitihani kufutwa ama kuahirishwa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo