ZAIDI ya vijana 79 waliokuwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kata ya Nzovwe, mkoani Mbeya, wamekihama chama hicho na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mbali
ya kupewa kadi za CCM, vijana hao walidai kuchoshwa na sera za CHADEMA
zinazohamasisha maandamano badala ya kuwajengea uwezo kiuchumi ili
waweze kujikomboa kimaisha.
Vijana
walipokelewa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa jijini humo, Bw. Charles
Mwakipesile, kufungua tawi lao la wateule Nzovwe ambapo vijana hao
walidai wamejipanga kukijenga chama hicho, kulinda amani na kujijenga
kiuchumi.
Awali,
Katibu wa vijana hao, Bw. Simon Charles, alisema vijana wengi waliopo
CHADEMA, wamekuwa wakitumika kuwanufaisha wanasiasa kwa kushiriki
maandamano ambapo mwisho wa siku, hupata ulemavu wa kudumu au kupoteza
maisha.
"Kwa
kutambua ukweli huu, tunaamini mustakabali wa maendeleo ya Watanzania,
bado uko mikononi mwa CCM ndio maana tumeamua kurudi kundini tukiwa na
malengo kudumisha amani, kujenga mshikamano thabiti ndani ya chama," walisema.
Akizungumza
baada ya kufungua tawi hilo, mgeni rasmi Bw. Mwakipesile, alisema hatua
waliyochukua vijana inapaswa kuigwa na vijana wengine waliopo CHADEMA.
Alisema
umefika wakati wa vijana kukataa siasa zenye mrengo wa chuki ambazo
hazisaidii kuwatoa katika lindi la umaskini ambapo chama tawala CCM,
kinafanya kazi kubwa ya kusimamia ilani yake ya uchaguzi, kudumisha
amani na utulivu nchini.
"Lazima
tujitafakari na kupinga vikali kauli za wanasiasa ambao wanahamasisha
maandamano lakini vijana ndio wanaoumia ambapo wao wanapanda ndege na
kwenda kupumzika Ulaya.
"Huu
ni unyama ambao lazima muukatae na kudumisha amani iliyopo ambayo ndiyo
matunda ya uhuru tulioupata...nawaomba Watanzania muunge mkono juhudi
zinazofanywa na Rais Jakaya Kikwete za kuleta maendeleo na kudumisha
demokrasia miongoni mwa wananchi," alisema.
