Mwanaume mmoja mkazi wa Kijiji cha Msimba wilayani Uvinza, Kigoma, anashikiliwa na Polisi akidaiwa kufungia watoto wake wanne ndani ya nyumba na kuwashindisha njaa kwa takribani miezi 10.
Ofisi
ya Ustawi wa Jamii, Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, iliwabaini watoto
hao hivi karibuni kijijini Sunuka, wilayani Uvinza. Kati yao, watatu ni
wa kiume.
Mkubwa ana umri wa miaka minane akifuatiwa na msichana mwenye umri wa miaka saba. Wengine wana umri wa miaka sita na minne.
Hayo
yalithibitishwa na Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kigoma, Penina Mbwete alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake na kumtaja baba mzazi wa watoto hao kuwa ni Mateso Hassan
(35).
Tayari
baba huyo anashikiliwa na Polisi ambapo awali ilikuwa katika Kituo cha
Ilagala kabla ya kuhamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi mjini Kigoma wakati
akisubiri kupandishwa kizimbani kusomewa tuhuma za kudaiwa kuwafungia
watoto hao na kuwazuia kwenda shule huku wakipata mlo mmoja tu, tena
usiku wa manane.
Mjomba
wa watoto hao, Sunday Zuberi (38) alidai mama mzazi wa watoto, Yauzia
Zuberi (38) alipigwa na mumewe na kuamua kukimbia akiwa na mtoto
mwingine mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja, ambaye pia alifariki baada
kuugua na kukosa matibabu sahihi.
Alisema
kwa kushirikiana na ndugu wengine na baadhi ya wanakijiji cha Msimba,
walifanya mpango wa kuwaokoa watoto hao na kumkamata baba yao.
Alidai
katika maisha yao ya ndoa, mama wa watoto hao alizuiwa kuhudhuria
kliniki wakati akiwa mjamzito hivyo watoto wake wote watano alilazimika
kujifungulia kwa wakunga wa jadi .
“Watoto wote hawakuwahi kutibiwa hospitali kwani baba yao alitaka watibiwe kwa dawa za kienyeji,” alidai Sunday.
Kwa mujibu wa Ofisa Ustawi wa Jamii Mbwete, watoto hao (majina tunayahifadhi) wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma, Maweni kwa uchunguzi wa kitabibu.
“Nitakachokifanya ni kuhakikisha kuwa baada ya tiba watoto hawa wanakuwa katika mikono salama. Natoa rai kwa ndugu yeyote ambaye ana uwezo, kukaa nao, lakini wawe salama…baada ya hapo tutakuwa tukiwatembelea kuhakikisha kuwa kweli wanaendelea kuwa salama.” alisisitiza Mbwete.
Kwa mujibu wa Ofisa Ustawi wa Jamii Mbwete, watoto hao (majina tunayahifadhi) wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma, Maweni kwa uchunguzi wa kitabibu.
“Nitakachokifanya ni kuhakikisha kuwa baada ya tiba watoto hawa wanakuwa katika mikono salama. Natoa rai kwa ndugu yeyote ambaye ana uwezo, kukaa nao, lakini wawe salama…baada ya hapo tutakuwa tukiwatembelea kuhakikisha kuwa kweli wanaendelea kuwa salama.” alisisitiza Mbwete.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Makris Yakayashi alisema baada ya
uchunguzi wa kitabibu, imebainika watoto hao wanakabiliwa na upungufu
mkubwa wa damu, utapia mlo mkali na matatizo mengine ya kisaikolojia na
upungufu wa kinga unatokana na kutopata lishe ya uhakika.
Mama
mzazi wa watoto hao, Gauzia Zuberi alisema katika maisha yao ya ndoa,
mumewe alikuwa akiwatesa kwa kuwapiga, kuwanyima chakula na wakati
mwingine kuwamwagia maji akidai anawaogesha kisha kuwatembeza mtaani
usiku kucha.
Credit: Habari leo
Credit: Habari leo
