AMNG'ATA MIDOMO MPENZI WAKE KWA KUMHISI ANA MCHEPUKO FACEBOOK




Huffington Post limeripoti habari kutoka Uingereza ya kusikitisha ya kijana Rhys Culley kumng’ata vibaya midomo mpenzi wake Chanttelle Ward mwenye umri wa miaka 18 wakati anamkiss baada ya kuwa na ugomvi unaohusisha na wivu wa mapenzi.
 
Kijana huyo wa miaka 23 alikuwa na wasiwasi baada ya kuhisi kuwa mpenzi wake alikuwa anachat na mwanaume kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook akimsaliti.
 
Akisimulia mkasa huo mbele ya jopo la majaji, Chanttelle ameeleza kuwa baada ya kutoka kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mama yake msichana huyo walielekea nyumbani kwao ambapo Rhys alianzisha mzozo akimtuhumu kuwa anamsaliti kupitia Facebook.
 

Kijana huyo alichukua simu ya Chanttelle kwa makubaliano ya kuangalia jumbe alizokuwa anatuma Facebook lakini hakukuta mawasiliano kati ya msichana huyo na mwanaume aliyekuwa anamhisi. Moja kwa moja akaanza kupaza sauti kwa hasira akidai kuwa amezifuta.
 
Hasira za kijana huyo zilimuogopesha akaona ni bora ampigie simu mama yake lakini alinyang’anywa simu. Rhys alifunga mlango na kuendelea kumshambulia kwa maneno.
 
Chanttelle anaeleza kuwa mgogoro huo ulipofikia hatua ya kupoa hivi, kijana huyo alimkiss huku akimuuliza kama kweli ana mpenda na hapo ndipo kila kitu kilibadilika.
 
“Aliweka mdomo wake wote kuzungumguka lips zangu na kuvuta, nilidhani lips zote zimetoka. Damu zilisambaa kila sehemu.” Msichana huyo alieleza.

Polisi walipofika walikuta wote wametapakaa damu usoni, wakamkamata kijana huyo na kumkimbiza Chanttelle hospitali huku akiwa na mikwaruzo katika sehemu mbalimbali za mwili.
 
Mwanaume huyo alipopewa nafasi ya kujitetea mahakamani hapo, alieleza kuwa hakuwa na nia mbaya ya kumuumiza mrembo wake ambaye anadai alikuwa na bahati kuwa naye.
 
Rhys alikutwa na hatia. Alirudishwa rumande na anasubiri hukumu yake mwezi ujao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo