AKUTWA AMEJINYONGA JUU YA MTI NA MWILI WAKE KUHARIBIKA VIBAYA, POLISI WAAMURU UZIKWE


Mwanaume  mmoja  mkazi  wa  Kiseke, Ilemela  jijini  Mwanza  amekutwa  amekufa  baada ya  kujinyonga  kwa  kamba  juu  ya  mti  huku  mwili  wake  ukiwa  umeharibika  vibaya  na  kuvuja  maji....

Inakadiriwa  kuwa  mtu  huyo  alijinyonga  siku  tatu  zilizopita  na  chanzo  cha  kifo  hicho  bado  hakijafahamika  kutokana  na  mtu  huyo  kutoaacha  ujumbe  wowote  huku  wakazi  wa  eneo  hilo  wakishindwa  kumtambua  vizuri  kutokana  na  mwili  wake  kuharibika.

Kutokana  na  hali  hiyo, maafisa  wa  jeshi  la  polisi  waliokuwepo  eneo  la  tukio  waliamuru  mwili  huo  uzikwe  baada  ya  uchunguzi  wa  awali  wa  daktari  aliyekuwepo  eneo  la  tukio.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo