skip to main |
skip to sidebar
UKATILI WA AINA YAKE: WATOTO WATATU WABAKWA KWA ZAMU!
Watoto watatu ambao ni majirani wamejikuta
wakiingia kwenye kadhia ya kubakwa kwa zamu na watoto wenzao ambapo
mmoja anadaiwa kuwa na umri wa miaka 17 huku mwingine akiwa na umri wa
miaka 14 ambaye pia ni denti wa darasa la nne.
Watoto watatu wadogo waliobakwa kwa zamu na watoto wenzao.
Tukio hilo la aina yake lilijiri hivi karibuni maeneo ya
Mbagala-Mianzini jijini Dar ambapo awali ilidaiwa kuwa wazazi wa watoto
hao walishtushwa walipogundua watoto wao wameingiliwa na kuharibika
vibaya baada ya kuwakagua kila mmoja kwa wakati wake walipokuwa
wakiwaogesha.
Wazazi wa kiume wa watoto hao.
Wakizungumza kwa masikitiko kwa nyakati tofauti,
wazazi wa watoto hao walidai kwamba walipowabana waliwataja kwa majina
waliowafanyia vitendo hivyo, jambo lililowafanya ‘kuwataiti’ watuhumiwa
kwani walikuwa wakiwafahamu.
Wazazi hao walidai kwamba walipowauliza watoto hao walikiri
kuwaingilia wenzao kwa zamu kwenye jumba bovu (pagala) ambapo walienda
mbali zaidi na kusema kuwa walikuwa wamewafanyia vitendo hivyo kwa muda
mrefu sasa kwa zamu, nyakati ambazo watoto hao walirejea kutoka shuleni
chekechea (jina kapuni kimaadili).
Wazazi wa kike wa watoto hao.
“Nilishtuka na kuumia sana baada ya kugundua mwanangu ameingiliwa, tena kwa kipindi kirefu kiasi kwamba ameharibika kabisa.
“Huwezi kuamini mke wangu alipopata taarifa alipandwa na presha kiasi
cha maisha yake kuwa hatarini,” alisema mmoja wa wazazi hao
aliyejitambulisha kwa jina moja la Hussein.
Waraka(RB) wa polisi wa kukamatwa kwa watuhumiwa.
Kwa pamoja wazazi hao waliripoti ishu hiyo kwenye Kituo cha Polisi
cha Charambe na baadaye Mbagala-Kizuiani ambapo majalada ya kesi hizo
yalisomeka MBL/RB/9608/14-KUBAKA, CHAR/RB/1292/2014-KUBAKA CHAR/RB/2192/2014-KUBAKA ambapo watuhumiwa wanasubiri kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
CHANZO:GPL
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi