Mwanamitindo Jessie Nizewitz ambaye alikuwa kati ya wasichana waliokuwa kwenye mashindano ya series ya ‘Dating Nak8d’ amefungua mashitaka dhidi ya makampuni yanayowezesha show hiyo kwa kurusha vipande vinavyomuonesha akiwa mtupu bila kuficha sehemu zake za siri.
Katika shitaka hilo, Jessie anadai fidia ya $10 million kutoka kwa
makampuni ya Viacom, Firelight Entertainment, Lighthearted Entertainment
kwa kushindwa kuficha kwa kuweka blur kwenye maeneo ya sehemu zake za
siri kama walivyokubaliana awali.
“Ingawa niliingia kwenye shindano hilo nikijua kuwa ningeshuti nikiwa
mtupu, niliambiwa kuwa sehemu zangu za siri zingefichwa kwa kuwekewa
blur kwa ajili ya show ya TV…hata washiriki wengine hawakutegemea kuona
hivyo.” Alisema Nizewitz.


