BATULI amesema kuwa anahitaji kwenda kusomea uhudumu wa ndege lakini anashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya kubanwa na maisha, lakini endapo atapata mtu wa kumlipia ada yupo tayari kuachana na filamu na kwenda kusoma.
Mrembo
huyo akizungumza na mwandishi hivi karibuni aliweka wazi ishu
hiyo kwa madai kwamba anahitaji kutimiza ndoto yake juu ya
suala hilo kwani ni wazo lake la muda mrefu ingawa hakuwahi
kumwambia mtu yeyote....
"Napenda
sana kazi hiyo ikibidi hata urubani kabisa pia naona naweza
kufanya.Tatizo ni gharama, naamini endapo ntapata mtu wa
kunidhamini naweza kwenda kusomea ili nitimize ndoto zangu za
muda mrefu,"alisema