Maiti za watu 13 kati ya 16 waliokufa katika ajali ya mabasi yaliyogongana juzi mkoani Tabora, zimetambuliwa na ndugu zao.
Ajali
hiyo ilitokea juzi saa 8 mchana katika kijiji cha Mlogolo wilaya ya
Sikonge baada ya basi ya Am Coach na Sabena kugongana uso kwa uso na
kusababisha vifo hivyo na majeruhi 81.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Suzan Kaganda alitaja waliokufa na maeneo
yao ya makazi ni Patrick Fumbuka , Fred Alex, Emmanuel Senga na Mabaga
Benedicto Peter.
Wengine
ni Nicholaus James, Mkazi wa Geita, Aristideth Shirima dereva wa basi
la AM Coach na dereva wa basi la Sabena, James Komba aliyekatika kichwa
na kutengana na mwili kwa kukatwa na bati.
Kamanda alitaja wengine ni Jacklini Lumendika, Nasma Zenda pomoja na mtoto wa kiume.
Alisema
katika basi hilo pia kulikuwa na wanafunzi waliokuwa wanakwenda kufanya
mtihani katika chuo cha kilimo Tumbi mkoani Tabora wakitoka Mbeya na
Iringa ambao ni Anna Kalimo na Joyce Mgeni.
Kaimu
Mganga wa Wilaya ya Sikonge mkoani hapa, John Buswelu alisema hadi
jana, majeruhi 63 waliruhusiwa kutoka katika hospitali ya wilaya hiyo na
wengine watatu wanapelekwa Tabora kwa ajili ya matibabu.
Hospitali ya Mkoa Kitete ilipokea wagonjwa wapatao 18 ambao ilionekana hawawezi kutibiwa katika hospitali ya Sikonge.
Akizumzumza
na waandishi wa habari jana, Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo ya mkoa
wa Tabora, Deus Kitapondya alitaja majina ya majeruhi.
Nao
ni Meena Shilindye, Silvesta John, Nyorobi Masaga, Salum Hamisi,
Athumani Jafari, Samweli Asubisye, Mgeta, Josephat Weya, Paulo Nyanda,
Amos Dominick, Joseph Msumari na Scola Kadati.
Wengine
ni Jenifa Sanga,Tora Mbilinyi, Sikujua Saimon na mtoto mwenye umri wa
mwaka moja ambaye mzazi wake alifariki. Pia yuko ambaye hawezi kuongea
kutokana na ububu.
