Mtu
mmoja ambaye hajatambulika amekutwa ameuawa kwa kuchomwa chomwa sehemu
mbalimbali za mwili wake na kitu chenye incha kali katika makaburi ya
misuna Singida mjini.
Wakielezea
tukio hilo balozi wa mtaa wa mwenge Bi. Mary Mwambusu na mwenyekiti wa
mtaa wa misuna Bwana Sarota Masawe wamesema tukio hilo linaonekana
kutokea majira ya alfajiri ya siku ya tarehe tano mwezi wa nane katika
makaburi ya misuna.
Viongozi
hao wa mtaa Mwenge na Misuna wamesema tukio hilo ni la kwanza kutokea
lakini wameliomba jeshi la polisi kuimarisha ulinzi hasa maeneo kama
hayo ilikudhibiti mauaji kama hayo yasi tokee tena.
Akiongea
kwa njia ya simu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida Bwana
Geofrey Kamwela amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika eneo la
makaburi yaliyopo misuna Singida mjini na amesema jeshi lake bado
linaendelea na uchunguzi kuweza kubaini chanzo cha mauaji hayo ambayo ni
ya kinyama.