skip to main |
skip to sidebar
AIBU: MSANII WA BONGO FLEVA ANASWA LAIVU AKINUNUA NGONO KWA MAKAHABA USIKU WA MANANE....!!!!
WAKATI wasanii wakitakiwa kuwa mstari wa mbele
katika kuenzi maadili mema kwa jamii ya Kitanzania, mambo yamekuwa
kinyume, baada ya nyota wa muziki wa kizazi kipya, Ramadhan Shaban
'Wabibi' kukutwa live, akipatana bei na wanawake wanaojiuza katika eneo
maarufu kwa machangudoa la Sinza Africasana jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki iliyopita.
Nyota
wa muziki wa kizazi kipya, Ramadhan Shaban 'Wabibi' akitega 'mingo'
kujiopolea machangu maeneo ya Sinza Africasana jijini Dar.
Wabibi anayetamba na kibao chake cha Kitenge kwenye vituo mbalimbali
vya redio na runinga nchini, usiku wa saa saba alikuwa akivinjari katika
viwanja hivyo, akichagua kama wafanyavyo wateja wa nguo dukani.
Mara baada ya kuonekana kwa msanii huyo katika viwanja hivyo, chanzo
chetu ambacho ni kikereketwa cha maadili, kilipiga simu katika ofisi za
Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kitengo kilicho chini ya Global Publishers
saa saba usiku kikiripoti skendo hiyo ya aibu.
Msanii Ramadhan Shaban 'Wabibi' akipatana bei na mmoja wa machangudoa.
Bila kuchelewa paparazi wetu alifika eneo la tukio kwa pikipiki na
kumkuta staa huyo akiendelea na chaguachagua yake kwa akinadada
waliovalia kihasara ili kuwavutia wanaume wakware.
Mwanga wa kamera
zetu hata hivyo haukuonekana kumshtusha sana msanii huyo ambaye
alijichekesha na kujifanya kuendelea na shughuli nyingine, kama
walivyokuwa wakifanya watu wengine katika eneo hilo linalosifika kwa
biashara ya ukahaba jijini Dar.
Ramadhan Shaban 'Wabibi' akiwa na changudoa mwingine.
Baada ya kujipatia picha za kutosha za tukio hilo na kuondoka eneo
hilo, makamanda wa OFM hawakwenda kulala, bali waliendelea na uchunguzi
wao katika mitaa mbalimbali.Katika hali isiyotarajiwa, saa mbili
baadaye, msanii huyo kwa mara nyingine alikutwa na OFM akiwa anaendelea
na biashara yake ya sagulasagula ya machangudoa, lakini hivi sasa akiwa
amehamishia kambi katika eneo la Sinza ya Mapambano.
Akiwa amevutiwa na mwanadada mmoja na kuanza kufanya naye mapatano ya
bei, paparazi wetu alimuwahi kwa kumpiga picha, ambapo safari hii
alishtuka zaidi na chapchap, akachukua Bajaj na kutokomea.
'Wabibi' akikurupushwa na kamera zetu za Global katika eneo la tukio.
Wabibi aliwahi kuwa memba wa kundi la muziki la Suba Mkole,
akijulikana kama Wambua Classic ambao walitoa albamu iliyotamba kwa jina
la Sonde.
CHANZO:GPL
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi