WAZIRI WA FEDHA AKERWA NA HABARI ALIYODAI NI YA UONGO ILIYOCHAPISHWA KWENYE GAZETI DHIDI YAKE

Waandishi wa habari amabo ni watu muhimu kwa kupasha umma habari wametakiwa kufuata weledi wao wa kazi na kuwapasha wananchi habari za ukweli na si kutunga habari kwa lengo la kupotosha umma. 

Kauli hiyo imetolewa bungeni na waziri wa fedha Mh. Saada Mkuya wakati akitolea ufafanuzi habari iliyochapishwa na gazeti la Tanzania Daima la jana Ijumaa Juni 27, kuwa alimwaga chozi wakati alipobanwa na kamati ya bajeti(kamati ya chenge). 

Waziri Mkuya amesema taarifa hizo si za kweli na badala yake picha iliyowekwa kwenye gazeti hilo ikimuonesha akiwa analia ilikuwa ni wakati wa msiba wa aliyekuwa waziri wa fedha marehemu William Mgimwa. 

Amesema vyombo vya habari ambavyo vinaaminika vinatakiwa kutoa habari za ukweli na si kuupotosha umma, na kudai hakulia wakati akihojiwa na kamati hiyo kwani kila kitu kilienda sawa. 

Tazama habari ambayo waziri huyo amedai ni ya uongo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo