MAHAKAMA ya Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, imewakuta na kesi
ya kujibu watuhumiwa watano wanaoshitakiwa kwa tuhuma za kulawiti mtoto
wa kiume wa miaka 16 (jina linahifadhiwa) ambaye ni mwanafunzi wa
Shule ya Sekondari J.K Nyerere wilayani humo.
Watuhumiwa hao ni Charles Kiule maarufu kama Nguto, January Alhaj na
Patrick Sapisi, wakiwemo walimu wawili; Hadija Salum na Namwaka Mbwana
wote waliokuwa wakifundisha katika Shule ya Sekondari J.K Nyerere ambao
watapadishwa kwa mara nyingine kizimbani Julai 2, mwaka huu, kwa ajili
ya kuanza usikilizaji wa kesi hiyo.
Washitakiwa hao walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Emmanuel Njuu ambapo
ilielezwa kuwa mshitakiwa wa kwanza hadi wa tatu ambao ni Nguto, January na Patrick wanakabiliwa na kosa la kulawiti.
ilielezwa kuwa mshitakiwa wa kwanza hadi wa tatu ambao ni Nguto, January na Patrick wanakabiliwa na kosa la kulawiti.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Novemba 3 mwaka jana, saa 12 jioni
katika eneo la Lembeni, Wilaya ya Mwanga, washitakiwa hao kwa pamoja
walimwingilia kinyume na maumbile mwanafunzi huyo na kisha kumuingizia
karoti na matango katika sehemu zake za haja kubwa halafu
wakamlazimisha kula matunda hayo.
Washitakiwa hao pia wanakabiliwa na kosa la pili la kujeruhi, ambapo
ilielezwa mahakamani hapo kuwa kabla ya kutekeleza kosa la kwanza,
walimpiga kijana huyo kwa kutumiwa waya wa umeme na fimbo hali
iliyomsababishia maumivu makali mwilini.
Katika kesi hiyo namba 118 ya mwaka 2013, washitakiwa namba nne na
tano; Hadija na Mbwana ambao wote ni walimu katika shule hiyo,
wanakabiliwa na kosa la kuwashawishi washitakiwa namba moja, mbili na
tatu kufanya kitendo hicho.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa walimu hao waliwashawishi washitakiwa
kumfanyia kitendo hicho cha kinyama kama kulipa kisasi kwa kile
kilichodaiwa kuwa mwanafunzi huyo alitaka kumbaka mtoto wa mwalimu wake
(Hadija).
Upande wa mashitaka ukiongozwa na mwendesha mashitaka wa serikali,
Beatus John, uliwasilisha mashahidi nane huku upande wa utetezi,
mshitakiwa wa kwanza hadi wa tatu walijitetea wenyewe na wakili Rehema
Mtulya anawatetea washitakiwa wa nne na tano.
