Mkurugenzi wa shirika la MASUPHA Bi. Aida Chengula.
Imeelezwa kuwa
Matatizo ya ukeketaji na migogoro ya ndoa yamepungua wilayani Makete kutokana
elimu iliyotolewa kwa wananchi na shirika lisilo la kiserikali la MASUPHA wakishirikiana na The Foundation for
Civil Societies katika kata tano za wilaya hiyo
Akizungumizia kuhusu hilo mkurugenzi wa MASUPHA Bi Aida
Chengula amesema mradi huo uliokuwa unadhaminiwa na shirika la The Foundation For Civil Societies ambao umetekelezwa katika kata tano ambazo
ni Ukwama, Mang’oto,Kipagalo,Ikuwo,na
Mfumbi zote za wilayani Makete
Pia amesema mradi huo ulianza Decemba 27 mwaka 2013 “mradi
wetu tumeutekeleza katikakata tano ambapo kila kata tulimujengea uwezo kijana
mmoja kwaajili ya kutoa elimu kwa jamii inayo mzunguka kuhusiana na mambo sera
ya taifa ya Ukimwi,unyanyasaji wa kijinsia,na elimu kuhusu unyanyasaji wa
kijinsia hususan ukeketaji kwa wanawake”
Bi Chengula alielezea faida walizo zipata katika mradi huo
kuwa malengo yao yametimia kwani idadi kubwa ya
mambo waliyolenga yametekelezeka ikiwemo kupunguza idadi ya kesi za
migogoro ya kifamilia katika mabaraza ya usuluhishi katika kata tano ambazo mradi
ulikuwa unatekelezwa na kuongeza kuwa jamii ilikuwa haina elimu kuhusina na
mambo ya ndoa ambayo mpaka kiasi Fulani
imepungua kutoka kesi 5 hadi 8 kwa mwezi na kufikia kesi 1 hadi 2 kwa mwezi
Hata hivyo Bi Chengula ameiambia blog hii kuwa licha ya
mradi huo kuwa na mafanikio amezitaja changamoto za mradi huo kuwa ni pamoja na
watu kuwa na uelewa mdogo wakati wa warsha mbalimbali kwani wamekuwa wakitaka kulipwa fedha nyingi
“Makete kuna mashirika mengi yanayotoa elimu hivyo watu
wamekuwa wakilinganisha viwango vya posho kutoka katika mashirika mengine hivyo kufanya
mwitikio wa jamii kuwa mdogo”alisema Bi Chengula na kuongeza kuwa pia kumekuwa na changamoto ya pesa za mradi kutokufika kwa wakati.
Kwa upande wao vijana waliokuwa wakitoa elimu katika vijiji
vya kata zao walieleza kufurahishwa na mradi huo kwani licha ya kusaidia elimu kwa jamii pia wao wamejengewa uwezo ambao utawasaidia kujijengea familia bora
Muwezeshaji Neema Sanga.
“mradi huu umewasaidia wanajamii kubadilika kwa kiasi
kikubwa hapa katika kata yetu kumekuwa na tatizo la akina mama wenye umri mkubwa kujihusisha
na mapenzi na vijana wadogo jambo ambalo limekemewa na elimu imetolewa na kumekuwa
na mabadiliko kwa jamii hiyo”alisema Neema Sanga muwezeshaji kutoka katika kata
ya Ukwama
Naye Frojensia Sage
mwezashaji kutoka katika kata ya Nkondo
alisema kama kijana ametoa elimu katika kata hiyo na kumesadia kubadilika husasani suala
ukeketaji kwa wanawake ambapo mpaka sasa jamii hiyo imeweza kubadilika pia
aliongeza kuwa kumekuwa na changamoto za
za utekelezaji ikiwemo vitendea kazi
kama vipeperushi ambavyo vinaweza kusaidia jamii pia kujijengea utaratibu wa kupata elimu kupitia maandishi
kwani yanahifadhika kwa muda mrefu
Bw. Sage alisema pia viongozi wa maeneo husika wamekuwa hawatoi
ushirikiano kwa wawezeshaji hao hao
Na Riziki Manfred