TAARIFA YA POLISI YASEMA BOMU LILILOTUPWA ZANZIBAR LAUA NA KUJERUHI WATU 7 ZANZIBAR

Wakaazi wa Zanzibar wako katika hali ya wasiwasi baada ya  kushuhudia tukio lengine la  kuripuka bomu kwa viongozi wa dini huku safari hii likiua kijana mmoja na kujeruhi saba.
 
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa upelelzi na makosa ya jinai zanzibar Sacp Yussf Ilembo ameseme bomu hilo la kutupwa na mtu au watu wasijulikana ambao walikuwemo ndani ya gari lilkuwahalina  namba za usajili lilitupa bomu hilo kwa kikundi cha wananchi waliokuwa pamoja na viongozi wa dini amabo walikuwa wametoka msikitini na wamesimama nje ya gari  ndipo walipotupiwa bomu hilo na kijana mmoja Mohamed khatibu Mkombalaguha ambaye ni mkaazi wa pongwe tanga aliyekuja Zanzibar kwa ajili ya hitima kufariki hapo hapo na wengine saba akiwemo Sheik Kassim Mafuta kujeruhiwa huku jeshi la polisi  hadi sasa hawajakamata mtu yeyote.
 
Nao baadhi ya majeruhi Amed Haidar na mwanawe khalid Ahmed wakiongea wakiwa wamelazwa hosptali ya Alrahma wamesema hawajui wala hawakumuona mtu ailyerusha bomu hilo wao wameshtukia  mripuko mkubwa wakati wa saa mbili na nusu na kurushwa.
 
Hakuna taarifa yeyote iliyotolewa na seriklai wakati hili likiwa ni tukio la pili la kuripuka mabomu kutokozea hapa zanzibar katika kipindi cha miezi mine bada ya mezi wa februari mabomu zadi ya matatu kuripuka katika mgahawa wa mercury na mabomu mawili nje ya lango kuu la kanisa la angilkana mkunazini na hadi sasa hamna mtu aliyekamatwa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo