RAIA WA NIGERIA AKAMATWA UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU JULIUS NYERERE AKIDAIWA KUMEZA KETE 100 ZA MADAWA YA KULEVYA

Mkuu wa Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa 
---
  Raia wa Nigeria, Anthony Ifeanyichukwa Okafor (52), amekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akidaiwa kumeza kete 100 za dawa za kulevya aina ya cocaine ambazo thamani yake bado haijafahamika.

Tukio hilo limetokea takribani siku 22 baada ya raia mwingine wa Nigeria, Olabisi Ibidun Cole (65) kuvunja rekodi ya umri wa watu wanaokamatwa wakiwa na dawa za kulevya katika uwanja huo.
 
Cole alikamatwa Jumatatu ya Mei 19, mwaka huu saa tisa alasiri akijiandaa kwenda Paris, Ufaransa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia, akiwa amemeza kete 82 aina ya heroini zilizokuwa zimefungwa kwenye karatasi zinazofanana na ganda la sigara, ambazo si rahisi kuonekana katika mitambo.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea.......


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo