NYOKA WA AJABU NA KUNDI LA NYUKI VYAWATOA MSITUNI BOKO HARAM

Wanajeshi wa Boko Haram wanaofanya mashambulizi na kuua raia wasio na hatia huko Nigeria linaelezwa kuanza kukimbia msitu baada ya nyoka wenye sumu kali na nyuki kuwashambulia.

Habari hizi zilielezwa na mtuhumiwa mmoja aliyekamatwa na kuthibitisha kuwa ni mmoja wa member wa kundi la Boko Haram na alieleza kuwa hivi sasa kundi hilo limelazimika kuhama msitu na linaelekea maeneo ya mpaka wa Nigeria na Cameroon baada ya wanajeshi wake wa ngazi za juu kushambuliwa na nyoka na kupoteza maisha.
Kumezuka hisia za kiimani kuwa Boko Haram wanaadhibiwa na mizimu ya watu waliokuwa waliowauwa kinyama.
Jeshi la Nigeria limeshafanya juhudi za kuwaondoa msituni lakini imeshindwa na hadi sasa kundi hilo linawashikilia wasichana zaidi ya 260 na bado linaendelea kushambulia Nigeria kwa mabomu ya kutegwa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo