MAHABUSU WAVUA NGUO NA KUBAKI UCHI KAMA NJIA YA KUHARAKISHWA KWA KESI ZAO WILAYANI GEITA

Katika hali isiyo ya kawaida mahabusu wa gereza la wilaya ya Geita waliofikishwa katika mahakama ya mwanzo ya nyankumbu kugoma kurudi mahabusu kwa kuvua nguo huku waking'ang'ania mlingoti wa bendera ya taifa kwa madai ya kushinikiza haki itendeke.

Mahabusu hao wamesema kuwa kila mara wamekuwa wakifikishwa mahakamani bila ya muafaka kupatikana huku wengine kesi zao zikimalizika haraka lakini hawajui kwanini wao kesi zao zinachelewa na kumtaka mkuu wa mkoa kuingilia kati suala lao ili kupatiwa ufumbuzi.

Ni malalamiko ya baadhi mahabusu hao ambao wanaona kukaa kimya kwa muda mrefu kunawafanya kutopata haki zao.

lakini ilibidi busara itumike ya kuwataka wavae nguo ili wasikilizwe kero zao.

mahabusu hao wamedai kuwa hawana nia ya kufanya fujo na kwakuwa serikali sikivu wanaomba kusaidiwa.

Katibu tawala wilaya ya Geita Gasper Kanyaita amechukua majina ya mahabusu hao ili kufatilia mafaili yao na kujua namna ya kuwasaidia.

Baada ya kubembelezwa kwa muda mrefu hatimaye mahabusu wakakubali kurudi gerezani baada ya kuahidiwa kuja kusikilizwa kero zao siku ya leo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo