"HOUSEGIRL" WA MIAKA 14 ADAIWA KUBAKWA NA MWAJIRI WAKE MKOANI MTWARA

MTOTO mwenye umri wa miaka 14, mkazi wa maeneo ya Mghalani, mkoaniMtwara, ambaye ni mfanyakazi wa ndani ‘Hausigeli’, anadaiwa kubakwa na mwajiri wake na kumsababishia maumivu makali.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Maisha Maganga, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Juni 16 na kwamba baada ya kufanya ukatili huo, mwajiri huyo aliyefahamika kwa jina moja la Sharifu, alitokomea kusikojulikana.

Kamanda Maganga alisema ili kufanikisha azma hiyo, mtuhumiwa huyo alitumia fedha kumlaghai mtoto huyo kisha kumbaka na juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Alisema Jeshi la Polisi linalaani vitendo hivyo viovu vikiwemo vya ubakaji na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watu wote watakaojihusisha na vitendo hivyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo