June 9 ilitoka rasmi video ya wimbo wa msanii wa kike wa Kenya aitwae
Sanaipei, unaoitwa Mfalme wa Mapenzi na ndani ya siku mbili tu
uliangaliwa YouTube zaidi ya mara 59,000.
Video hiyo iliyoongozwa na Mhando Brian imetabiriwa kufungwa
isichezwe kwenye vituo vya television vya Kenya kwa kuzingatia
kilichotokea kwa wimbo wa Sauti Sol, Nishike.
Mfalme wa Mapenzi inawezekana imeenda nje ya maadili hata zaidi ya
video ya wimbo wa Nishike wa Sauti Sol kwa kuzingatia vigezo
vilivyotajwa hadi kuifungia hiyo Nishike.
Sanaipei anaonesha jinsi ambavyo anaweza kupata faraja ya moyo kutoka
kwa mwanaume anaejua wapi pa kushika na nini cha kufanya wanapokuwa
faragha.
Hilo linaweza lisiwe tatizo, lakini tatizo linaweza kuwa jinsi alivyoonesha kwa vitendo na hisia kuhusu kile anachokizungumzia.
Hilo linaweza lisiwe tatizo, lakini tatizo linaweza kuwa jinsi alivyoonesha kwa vitendo na hisia kuhusu kile anachokizungumzia.
