Mwanamuziki Diamond amefunguka kuhusu madai ya baadhi ya wasanii kuwa aliwaibia idea au nyimbo zao na kuzifanya zake.
Ameeleza kuwa malalamiko yao hayana ukweli kwa kuwa kuna maneno
ambayo yamezoeleka na yanaweza kutumiwa na watu wote lakini anapoyatumia
hutokea msanii aliyetumia maneno kama yale na kudai kuwa ameiba idea
yake.
Ametoa mfano wa nyimbo kama Moyo Wangu ambao anasema baada ya kuimba
wasanii wengine waliimba pia lakini hakuwahi kujitokeza kusema ameibiwa
kwa sababu neno hilo linaweza kutumika na kila mtu kwa ufundi wake.
Diamond ameeleza pia kuhusu tuhuma za Wababa (ingawa hakumtaja jina)
kuwa alimuibia wimbo wake wa Kitorondo na sasa anauita Mdogomdogo.
“Sitaki niongee kwa sababu nitampa Kick…anyways nilisikia kuna
mtu anasema eti hii nyimbo yangu ya MdogoMdogo kuna mtu kaibiwa kwa neno
la Kitorondo. Sasa mimi nikuadithie story fupi…mimi nimezaliwa Tandale
nimekulia Tandale, kuna bendi ilikuwa inaitwa Tandale Modern Taarab
nyimbo yao ya kwanza inaitwa Tandale (anaimba kidogo). Ukiacha hivyo,
Kitorondo ni jina ambalo ni ngoma ambayo wanaimba hivyo (anaimba). Yaani
hii ni nyimbo.
“Kuna msanii kaichukua kaiimba kama ilivyo ile nyimbo ya
mdundiko. Halafu baada ya kusikia neno la Kitorondo kwenye nyimbo yangu
akasema yeye kaibiwa nyimbo. Mimi nimepata taarifa nikasema ana akili
kweli. Yeye ndio kaenda kuiba. Mimi nimetumia neno la Kitorondo kwa
taaluma zangu za kimuziki naliingiza kwa namna gani kama neno, yeye
anasema nimemuibia yeye. Sikujisikia vizuri…halafu nikaulizwa kila
sehemu nikienda nawaambia msiniulize maswali hayo kabisa.”