TRA NA COSOTA WAPEWA SIKU 5 WAANDAE STIKA MPYA ZA KUWANUFAISHA WASANII

Serikali imetoa siku tano kwa mamlaka ya mapato (TRA) na COSOTA kukaa pamoja na kutengeneza stika za kukusanya ushuru pamoja na za kulinda wizi wa kazi za wasanii. 

Naibu waziri wa fedha na uchumu Mh. Mwigulu Nchemba ametoa agizo hilo bungeni Dodoma hii leo wakati akijibu swali la Nyongeza la mbunge wa viti maalum Mh Martha Mlata. 

Mh. Mwigulu amesema si kweli wasanii na kuona kuwa kazi zao hazina maana, bali imekuwa ikijitahidi kutambua kazi zao na wao wanufaike na jasho lao na ndiyo maana ametoa agizo hilo. 

Mh Mlata alikuwa akilalamikia kuwepo kwa stika za TRA ambazo hukusanya ushuru tu lakini hakuna ukusanyaji mzuri wa stika unaonufaisha wasanii.

Na Edwin Moshi, Dodoma


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo