MSANII NATASHA WA BONGO MUVI NAYE AUGUA HOMA YA DENGUE

STAA mkongwe wa filamu Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ ameongeza listi ya mastaa ambao wameathirika na ugonjwa wa dengu (Dengue Fever).

Akipiga stori na mwandishi wetu, Natasha alisema tangu Rais Jakaya Kikwete aingie madarakani, hajawahi kuugua hata homa lakini kwa mara ya kwanza mwaka huu homa ya dengu imemlaza.

“Nilianza kusikia baridi kali sana kisha nikawa naishiwa nguvu na mishipa inakakamaa, nilihisi naaga dunia kiukweli lakini niliwahi kwenda hospitali, nimepata tiba, nimeruhusiwa na ninaendelea vizuri,” alisema Natasha.

Miongoni mwa mastaa ambao wameumwa ugonjwa huo ambao hauna tiba ya moja kwa moja ni Rehema Chalamila ‘Ray C’, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ na Miss Afrika Mashariki namba 2, 2008, Aneth John.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo