MAJANGA TENA: WANAMUZIKI 5 WA PEPETA HOI KWA DENGUE

HOMA ya Dengue imezidi kuwa tishio jijini Dar es Salaam, ambapo wanamuziki watano wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’, wamekumbwa na ugonjwa huo

Mtoa habari Hassan Rehani ambaye ni meneja wa bendi hiyo, alizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni na kuwataja wanamuziki hao kuwa ni Badi Bakule, Ramadhan ‘Pentagoni’, Bakari Kasongo ‘Mandela’, Sabrina Mbetembete na Natalia Mbui.

“Nimeshitushwa sana na ugonjwa huu, maana katika maisha yangu ugonjwa ambao nilishawahi kuona unasumbua watu wa sehemu moja kwa wingi kiasi hiki ni Kipindupindu tu,  sasa hii dengue ni hatari,” alisema Rehani na kuongeza kuwa wanamuziki hao walikuwa wamelazwa Hospitali ya Mwananyamala na kwamba hali zao zilikuwa zinaendelea vizuri.

Naye mmoja wa wagonjwa hao, Rama Pentagoni, alipozungumza na mwandishi wetu alisema anaendelea vizuri, huku akiuelezea ugonjwa huo kuwa ni hatari kwa afya ya binadamu.

CHANZO:Risasi Mchanganyiko.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo