Stori: Musa Mateja, GPL
MSANII mwenye sauti mwanana anayetesa kwenye Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’, amefunguka kuwa, ndoa yake na mpenzi wake Nagari Kombo ‘Kaka wa Bongo’ inanukia.
MSANII mwenye sauti mwanana anayetesa kwenye Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’, amefunguka kuwa, ndoa yake na mpenzi wake Nagari Kombo ‘Kaka wa Bongo’ inanukia.
Linah alisema hayo wikiendi iliyopita aliponaswa akijiachia na Kaka
wa Bongo katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar ambapo mpango mzima wa Tuzo
za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 – 2014 ulikuwa ukifanyika.
“Sina haja ya kuendelea kumficha mpenzi wangu, kwani kwa sasa
anatambulika kwa kila mtu na hasa ndugu zangu wa karibu, kitu cha
kusubiriwa kwa sasa ni tarehe ya ndoa yetu tu,” alisema Linah.
Kaka wa Bongo alijizolea umaarufu siku za nyuma baada ya kuingia
uwanjani na kumkumbatia mchezaji, Ricardo Kaka wa Timu ya Taifa ya
Brazil iliyokuwa ikichuana na Taifa Stars katika Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam.