
Jiwe kubwa Likiwa limeanguka toka mlimani na kuziba Barabara ya Vuga Kutoka Mombo kuelekea korogwe na Lushoto


Kwa juu ni mlima ambapo jiwe hilo liling'oka na kudondoka hatimaye kuziba barabara hiyo kwa takribani masaa sita

Abiria na madereva wakiwa wamekaa wakisubiri mamlaka zinazohusikka wafike ili kutoa msaada wapate kuendelea na safari.

Vyombo
vya dola wakiwa wamefika eneo la tukio tayari kuweza kulisogeza jiwe
hilo ili abiria na watumiaji wa barabara ya vuga kuendelea na shughuli
zao

Hayo ni baadhi ya mawe ambayo yanaonekana kwa juu ya barabara ya vuga inayounganisha kutoka mombo kuelekea lushoto.
Hali ya usafiri kutoka mombo-korogwe kuelekea wilaya ya Lushoto mkoani tanga ilikuwa tete baada ya jiwe
kubwa kuangua barabarani katika eneo la vuga road.Jiwe hilo
lilisababisha wasafiri wa barabara hiyo kukwama kwa takribani masaa 6
bila magari kupita.Lakini hatimaye baadae vyombo vya usalama
wakishirikiana na wanainchi waliweza kulitoa na hatimaye usafiri wa njia
hiyo kurejea katika hali yake ya kawaida.
Chanzo:Pamoja blog