Meya
wa jiji la Dar es Salaam,Dr Didas Massaburi amesema abiria
wataokutwa wakiwa wamepanda Pikipiki maarufu kama Boda boda
katika maeneo ambayo pikipiki hizo hazina leseni ya kufanya
biashara watakamatwa na kufikishwa mahakamani pamoja na
dereva.....
Alisema
pia wafanyabiashara wadogo wataokutwa wakifanya biashara katika
maeneo yasiyoruhusiwa kisheria ikiwemo maeneo ambayo yamefanyiwa
usafi na Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam hivi karibuni
watakamatwa na kufikishwa mahakamani.....
Meya
huyo aliyasema hayo jijini Tanga hivi karibuni alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari ambao walitaka kufahamu
msimamo wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania ( ALAT )
kuhusu kunyanyaswa kwa waendesha bodaboda katika maeneo
mbalimbali nchini
