Ama kweli kila nyuma ya mafanikio ya mwanaume kuna mwanamke imara.Hili limejidhihirisha mwishoni mwa wiki iliyopita wakati msanii kiwango wa bongo fleva Naseeb Abdul 'Diamond Plutnumz' alipoweka rekodi ya msanii aliyechukua tuzo nyingi za Kili Music tangu tuzo hizo zianzishwe.....
Diamond
akiwa ameongozana na mpenzi wake Wema Sepetu kwenye tuzo hizo
zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar
alionekana kuwa na furaha muda wote wakati wa kwenda kuchukua
tuzo hizo....
Diamond
alizoa tuzo 7 na kuacha gumzo ikiwa ni mafanikio yake
makubwa kuwahi kuyatapata tangu tuzo hizo zianzishwe akiivunja
na kuipita rekodi ya 20% aliyewahi kuchukua tuzo 5 mwaka
2011....
Akiongozana
na mpenzi wake katika kila tuzo, Diamond alikiri kuwa tuzo
hizo ni kwa ajili ya baby wake huyo ( Wema ) huku akimshukuru
pia mama yake na kampani yake....
Ni
muda sasa uhusiano kati ya Wema na Diamond umekuwa ukigonga
vichwa vya habari katika sura tofautitofauti huku wawili hao
wakiendelea kupambana na hali hiyo....
Wema ameonekana kujirekebisha kwa wakati huu ambao amerudiana na Diamond tofauti na walivyokuwa awali....
Uhusiano
wao umeteka hisia za watanzania wengi kutokana na matukio
mengi yanayowaandama ikiwemo mama Wema kuingilia mapenzi yao na
pia mama Diamond kutopendezwa na uhusiano huo huku
akipendekeza Penniel Mungilwa 'Penny' kuwa mpenzi wa mwanae....
Watu
wa karibu na Diamond wanaopingana na mama Diamond huku
wakimpendekeza Wema wamedai kuwa Wema Sepetu ana kismati na
Diamond tofauti na ilivyo kwa Penny....
Wakiendelea
kufunguka, watu hao waliweka wazi kuwa wakati wote Diamond
anapokuwa na Wema hung'aa tofauti na alivyokuwa na Penny
ambapo kila kitu kilirudi nyuma....
"Nakwambia
Diamond asingecheza karata dume ya kurudiana na Wema,sasa hivi
angekuwa katika hali mbaya sana,sema nina msifu anaakili za
kuzaliwa na anajua kusoma alama za nyakati" Alisema ndugu mmoja aliyekataa kuandikwa jina lake
Akifunguka
hivi karibuni, mtangazaji mmoja wa redio maarufu hapa nchini
ameeleza kuwa hata tuzo alizopata Diamond, Wema anahusika kwa
kuwa anamvuto wa ajabu....
"Diamond
sasa hivi hana haja tena ya kwenda kwa waganga, maana kuna
tetesi hizo.Wema ni kama hirizi yake,yaani kila anapogusa ni
balaa.Huyo Penny kama alikuwa anasubiria kuolewa atasubiria
miaka mia" alimalizia mtangazaji huyo
