Meneja mahusiano wa serikali wa Nmb kanda kutoka Mbeya bw. Focus Lubende (kushoto) akimkabidhi msaada wa mashuka mgeni rasmi, kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete Bw. Cyrus Kapinga
Benki ya NMB Tawi la Makete wametoa msaada ya mashuka 90, katika hospitali ya wilaya ya Makete mkoani Njombe ikiwa ni mchango wao kama wadau wa huduma za afya wilayani hapo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani, Meneja mahusiano wa serikali wa Nmb kanda kutoka Mbeya bw. Focus Lubende amesema wao kama wadau wanatambua mzigo mkubwa ilionao serikali katika kuboresha huduma za afya hivyo wamelazimika kufanya hivyo ili kusaidia kuboresha huduma za afya wilayani Makete.
Bw. Lubende amesema wanawaomba watumishi wa afya kuyatunza mashuka hayo ili yakae muda mrefu kwa ajili ya kusaidia wagonjwa mbalimbali wanaofika kwa ajili ya matibabu katika hospitali ya wilaya ya Makete.
"Haitakuwa vizuri kwamba ndani ya wiki mbili ama tatu mashuka haya yakjawa yamechakaa yaani hayafai tena, tunaomba myatunze na yatumike kwa malengo husika" amesema.
Meneja wa Nmb Makete amesema msaada huo umetolewa na NMB Makao Makuu kwa ajili ya mkoa mzima wa Njombe hivyo mashuka hayo 90 ni miongoni mwa mgawanyiko kwa hospitali zote za serikali mkoani hapa.
Akishukuru baada ya kukabidhiwa msaada huo Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Bw. Francis Chaula (pichani) amesema mashuka hayo yatatunzwa vizuri na yatadumu muda mrefu kwani wanathamini sana michango ya wadau.
Chaula amesema wao kama viongozi watahakikisha pia yanafanyiwa usafi ili wagonjwa watakaoyalalia mashuka hayo wasiopate tabu huku akiwaomba wadau wengine kujitokeza kuunga mkono jituhada hizo za NMB Makete ili kwa pamoja waboreshe sekta ya afya