skip to main |
skip to sidebar
WATOTO WA FAMILIA MOJA WAFA PAMOJA KWA KUUNGUA MOTO WAKIWA WAMELALA
Stori: Juma Kapipi, Tabora
INAUMA sana! Watoto
wawili wa kiume wa familia moja, Daniel Paul (8) na mdogo wake, Emmanuel
Paul (3), wamepoteza maisha wakiwa pamoja baada ya kuteketea kwa moto
ndani ya nyumba.
Miili ya watoto wawili, Daniel Paul na mdogo wake, Emmanuel Paul ikitolewa eneo la tukio.
Katika tukio lililojiri majira ya saa 1:00 asubuhi, maeneo ya Mtaa wa
Rufita, Mwanza-Road mjini hapa baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi
kuteketea kwa moto huku wakiwa wamelala ndani.
Habari za awali zilieleza kuwa chanzo cha moto huo kilidaiwa kuwa ni
hitilafu ya umeme na kuisababishia familia hiyo majonzi makubwa ya
misiba miwili kwa mpigo.
Kulia ni mama wa watoto Daniel Paul na mdogo wake, Emmanuel Paul akilia kwa uchungu.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Tabora, OCD, Samwel Mwampashe
alithitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiahidi kuwa polisi watafanya
uchunguzi ili kubaini chanzo kamili cha moto huo.
CHANZO:GPL
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi