WATU watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma kwa kufanya mkusanyiko usio halali huku wakiwa wamebeba mabango yanayohamasisha uvunjifu wa amani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) David Misime alisema tukio hilo lilitokea jana katika maeneo mawili tofauti.
Aliwataja waliokamatwa katika tukio hilo ni Augustino Pancras (60), mkazi wa Kilimani, Cosmas Katebeleza (44), mkazi wa Kikuyu na Jotam Tarukundo (44) mkazi wa Chidachi.
Kamanda Misime alisema mmoja ya mabango waliyokamatwa nayo yalikuwa na ujumbe ufuatao: "Wajumbe msijivunie wingi wenu humo ndani sisi wananchi tupo nje na ndiyo wengi maoni yetu yaheshimiwe"
Alisema watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na Jeshi la Polisi na upelelezi ukikamilika kulingana na ushahidi watafikishwa mahakamani kwa kufanya mkusanyiko usio halali na kuwa na mabango ya kuhamasisha uvunjifu wa amani.
Bado Polisi wanaendelea kuwatafuta watu wengine waliokimbia.
Habari za kuaminika zilizopatikana zinasema mtuhumiwa moja Katebeleza alikamatwa eneo la Dodoma hoteli akiwa amebeba bango.
Huku watuhumiwa wengine wawili Pancras na Tarukumbo wakikamatwa katika eneo la hoteli ya St. Gasper ambapo kwenye maeneo yote waliyokamatiwa Wajumbe wa bunge maalum la katiba wapo kwa ajili ya kujadili rasimu.
Hata hvyo bado haijafahamika lengo la watuhumiwa hao kuandamana wakiwa na mabango.
via Lukwangule blog