Vijana wakiwa kwenye
matembezi ya Uzalendo yalioratibiwa na Umoja wa Vijana wa CCM katika
kuadhimisha miaka 50 ya Muungano ambapo vijana hao walianzia matembezi
kutoka ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Temeke mpaka kwenye viwanja vya
sabasaba na kulakiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
Vijana wakionyesha uzalendo kwa kuonyesha skafu zao zenye jina la Tanzania
Ujumbe maridhawa ambao ndio gumzo la mjni kwa sasa.
Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhani Madabida muda mchache kabla ya
kupokea matembezi ya Uzalendo yaliofanywa na vijana mbali mbali.
Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Sadifa Juma Khamis akienda kukabidhi bendera ya Taifa kwa Dk Jakaya Mrisho Kikwete .
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameshikilia picha
ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage huku Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwa ameshikilia picha ya
Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume baada ya kuzipokea
kutoka kwa vijana waliofanya matembezi ya Uzalendo.





