skip to main |
skip to sidebar
HUYU NDIYE MWANAMKE MREMBO ZAIDI KWA MWAKA HUU 2014
Lupita Nyong'o mwanamke mrembo zaidi duniani mwaka 2014.
Jarida la People limemtangaza Mkenya Lupita Nyong’o kama mwanamuke mrembo zaidi duniani mwaka 2014.
Lupita ambaye alishinda tuzo ya Oscar kwa uigizaji wake katika filamu
'12 years a slave,' yuko kwenye ukurasa wa juu zaidi wa makala ya wiki
hii ya jarida hilo.
Katika
orodha yake ya wanawake 50 warembo duniani,Lupita amewapiku waigizaji
maarufu akiwemo Kerry Washington, ambaye pia alishiriki katika filamu
hiyo na mwanamuziki Pink ambao walikuwa katika nafasi ya 10 na 5
mtawalia.
Jarida la People limemtaja Lupita kuwa mwanamke mrembo
Stacy Kiebler ambaye alisifika sana kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi
na muigizaji nyota George Clooney, alishikilia nafasi ya nane.
Hatua
ya Jarida la People ambalo huchapishwa kila wiki nchini Marekani na
kusomwa na karibu watu milioni 40, kumkubali Lupita kama mwanamke mrembo
duniani, ni kama tuzo kivyake kwa muigizaji huyo ambaye amegonga vichwa
vya habari nchini Marekani tangu kushinda
Mtandao wa People.com, unasema kuwa muigizaji huyo alifurahia sana
kutajwa na jarida hilo kama mwanamke mrembo hasa kwa sababu wasichana
kama yeye watapata kuwa na matumaini ya kufanikiwa maishani kama yeye.
"Nimefurahi sana na hii ni fursa kuwafanya wasichana wengine wajihisi kuwa wana uwezo wa kufiia chochote maishani mwao.
CHANZO NI BBC SWAHILI
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi