Pichani ni Mkurugenzi pamoja na viongozi
wa Shirika la HakiElimu wakitoa tamko hilo kwa waandishi wa habari.
Serikali imekuwa ikiajiri walimu kila mwaka, na hivi karibuni imetangaza
ajira za walimu 36,021.
Kati ya hao, walimu 17,928 ni kwa ajili ya
shule za msingi na walimu 18,093 ni kwa ajili ya shule za sekondari.
HakiElimu imefanya uchambuzi wa ugawaji huo wa walimu kimikoa kwa elimu
ya msingi na kugundua kuwa kuna mapungufu katika ugawaji huo
uliofanyika.
HakiElimu inaamini zoezi hili lingefanyika kwa usawa basi
elimu ya msingi ingefikia lengo la kitaifa la uwiano wa mwalimu mmoja
kwa wanafunzi 40.
Fungua linki ifuatayo http://bit.ly/PhtmZq ili kupata uchambuzi kamili wa mapungufu yaliyopo na mapendekezo kutoka katika Shirika la HakiElimu.