Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amewaambia Wananchi wa Tanga, jana tarehe 27
Machi,2014 wakati akihutubia Mkutano wa hadhara katika barabara ya
Karume kuwa;
"Tayari
Halmashauri za Mkinga, Pangani na Kilindi zimeshapata pesa hizo , na
tumetenga kiasi kama hicho kwa kila Halmashauri zingine nchini ili
kuboresha makazi na Nyumba za Walimu " Rais amesema.
Fedha hizo ni sehemu ya fedha iliyotengwa maalum na Serikali kwa
ajili ya kujenga nyumba za walimu katika Halmashauri arobaini na moja
(41) nchini kote katika kipindi cha Mwaka wa fedha wa 2013/14.
Halmashauri zingine zitakazofaidika na mpango huo ni Mlele, Nsimbo ,
Meatu, Makete, Ngorongoro na Longido. Pia Halmashauri za Bagamoyo,
Mafia, Kisarawe, Rufiji,, Kigoma, Kasulu, Kibondo, Nachingwea, Kilwa,
Liwale,Ruangwa Rorya, Chunya, Ileje, Rungwe, Kilombero, Ulanga, Newala,
Tandahimba na Nanyumbu zitafaidika na mpango huo wa Serikali.
Aidha, Halmashauri za Ukerewe, Sengerema, Kwimba, Tunduru, Namtumbo na Sikonge pia zimo katika mpango huo wa Mwaka huu wa fedha.
Halmashauri
za Muleba, Ngara, Nkasi, Kiteto na Simanjiro nazo zimo katika mpango
huu ambao Serikali imedhamiria kuutekeleza ili hatimaye kuwatengenezea
mazingira mazuri walimu hapa nchini.
Rais
amemaliza awamu ya kwanza ya ziara yake ya kikazi Mkoani Tanga ambapo
ametembelea, kukagua shughuli za maendeleo na kufungua miradi ya
Barabara, Maji, Soko na Maabara Mkoani Tanga.
Katika ziara
yake hiyo Rais ametembelea Wilaya za Handeni, Korogwe, Muheza na Tanga
ambapo katika awamu ya pili Rais amepanga kutembelea Mkinga, Lushoto,
Kilindi na Pangani.
Rais amerejea jijini Dar es Salaam jana jioni.
Imetolewa na;
Premi Kibanga
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Tanga.