MOTO WATEKETEZA NYUMBA YA MKUU WA WILAYA KILWA

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhd1GXRdMVoUZ2VyT8ay8OpR2SU_WhbOpj2sbLWgo4u17SX7uVxB4bbVwKVjE8Dzf6CMVjQ-q3MMNuJoYPMOeZzuH3CFm2AgT9mhV9_eJewlqIj-54ISEHyqEXukUsbgJXW1H6srn97UeXN/s1600/526079ec53737c3f5c833c0e87afd0d0.jpgNa Abdulaziz Video,Kilwa

Moto umeteketeza nyumba anayoishi mkuu wa wilaya ya Kilwa,mkoani Lindi, Mhe. Abdallah Ulega na kusababisha hasara kubwa ambayo idadi yake haijaweza kufahamika mara moja. 

 Habari kutoka wilayani humo na kuthibitishwa na Katibu tawala wa mkoa wa Lindi  Bw. Abdala Chikota alisema kwamba moto huo umeteketeza vifaa mbalimbali  ndani ya nyumba ya kiongozi huyo. 

 Bw. Chikota alisema moto huo umesababisha hasara kubwa. 

 Alisema kufuatia tukio hilo ofisi ya mkuu wa mkoa imetoa fedha Shilingi laki tano 500.000 pamoja na chakula kama mchele, unga sukari, mafuta ya kula pamoja na maharage ili kumsaidia DC huyo  katika kipindi
hiki cha majonzi wakati  utaratibu mwingine wa kutatua
tatizo la makazi yake ukifanyiwa kazi.


Mkuu wa wilaya huyo, Mhe. Ulega, alisema kuwa vitu vichache tu ndiyo vimeweza kuokolewa, ambavyo vilikuwa rahisi kuchukuliwa ikiweno begi la nguo na nyaraka zake, na kwamba kwa sasa atalazimika kuishi katika jengo la Hostel. 

 Mhe. Ulega ameshukuru  juhudi za wananchi ambazo zimesaidia kuokoa vitu vichache, vikiwemo seti ya makochi, magodolo matatu na kitanda kimoja cha mbao

Amesema wakati nyumba yake ilipokuwa ikiungua, familia yake akiwemo mke alikuwa safarini na amerejea leo mchana.

  Kwa upande wake kamanda wa polisi Regnal Mzinga amethibitiasha kutokea kwa tukio hilo n
a kueleza kuwa uchunguzi unafanyika ili kubaini chanzo cha moto huyo

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiu2EGzNE3RlATD9sgwtM4dVvN_JxHi95VPW_kvMBinS79c_G3WOPMzSNWz0iLsyQ3Fa98kwKvvIzzG4_YUuA9boVoBPYyyPHLA70W2FTWMk7L9JwZH9N0Ex_0ait1hS2GC-9CxslzIp-Ia/s1600/2bf48fd07329dfe68ba368fa23e2361b.jpgSehemu ya uani mwa nyumba hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo