Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara,Ndugu Philip Mangula akiongea na Waandishi wa Habari
Makamu
Mwenyekiti wa CCM-Bara,Ndugu Philip Mangula akiongea na Waandishi wa
Habari kutoka vyombo mbalimbali mapema leo asubuhi ndani ya Ofisi za
Makao makuu ya chama hicho,huku akiwaonesha picha iliyotumika kwenye
moja ya gazeti la kila siku hapa nchini,kwamba baadhi ya Wapinzani
wamekuwa wakitumia vibaya nafasi za kutafuta uongozi kwa kuwadhalilisha
watoto kupitia umaskini wao walionao ikiwemo sambamba na watu
wengine,jambo ambalo si haki na si sawa.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM-Bara,Ndugu Philip Mangula akiongea na Waandishi wa
Habari kutoka vyombo mbalimbali mapema leo asubuhi ndani ya Ofisi za CCM
mkoa wa Iringa,mara baada ya kuwasili mkoani humo.Mangula amesema kuwa
amekuja Iringa kuratibu na kuhakikisha kuwa chama chake kinamaliza
kampeni zake za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga kwa utulivu na
amani,akaongeza kuwa ingawaje wana taarifa ya baadhi ya watu wamejiandaa
kufanya fujo,lakini kwa bahati nzuri wameyapata majina ya watu
hao,"Majina hayo yako ishirini ntayataja hapo baadae ili wananchi kwa
ujumla wajue taarifa hizo ambazo zinapaswa kupingwa na kulaaniwa kwa
namna yoyote ile" alisema Mangula kwa msisitizo..
Pichani
kati shoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara,Ndugu Philip Mangula
akipokelewa na Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Mjini Ndugu,Hassani Mtenga
na wanachama wengine,alipokuwa akiwasili kwenye Ofisi za CCM mkoa wa
Iringa, mapema leo .