LIVERPOOL YAIUA MAN UNITED, YAIPIGA 3-0

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgpgjm5Zf2Ue6uG8qvGJLtQXUezW_PgiiS2vT8UQ6JvLyRddSvKXxU0ymobwimjIzi6n1N41gNRvqL8FEl7l9xrVHY2IvDdPNBXIh3S8TxEaAu1Dyds1WygZpLzRWZ95LccL9z5sagap8Hh/s1600/6906__7332__gerrard263_5325bd1fe5694524587035+(1).jpgLiverpool leo wameheza  kandanda safi ingine kwa miaka kibao kwa kuichabanga  Manchester United 3-0 katka
uwanja wao wa nyumbani wa  Trafford on
Sunday,  huku mkongwe asiyezeeka  Steven Gerrard akitikisa nyavu mara mbili kwa njia ya penati na kulihamasisha Bwawa la Maini kwa mara ingine tena.


Kiungo huyo alipiga penati mbili za kufa mtu kuhakikisha vijana wa Brendan Rodgers wakiondoka na pointi
tatu zote.

Luis Suarez aliongeza maumivi kwa Man U baada ya ‘chumba’ cha uhakika cha  Daniel Sturridge  kilipoguswa na kudondoka mbele yake,  ambapo raia huyo wa Uruguay hakufanya makosa alipochomeka kitu nyavuni mbele ya kipa wa Man U  David De Gea kumaliza kazi ya siku.

Ndio kusema Bwawa la Maini limechukua tena nafasi yake  pili (kuelekea ya kwanza) baada ya kuikopesha Manchester City kwa masaa kadhaa. Hadi sasa, kwa mujibu wa wataalamu wa soka,  hakuna sababu ya kulifanya Bwawa la Maini likose kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa mara ya 20!


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo