Hii ndio ‘Dear Leader’ style wanayotakiwa kunyoa wanaume wa Korea Kaskazini
Tumekuwa
tukisikia sheria mbalimbali zikipitishwa katika nchi mbalimbali
zinazowataka watu wavae au wasivae mavazi ya aina fulani, lakini huko
Korea Kaskazini imepitishwa sheria inayowataka wanaume wote wa nchi hiyo
kunyoa style ya nywele ya kiongozi wao iliyopewa jina la ‘Dear Leader’
Wiki
mbili zilizopita serikali ya Korea Kaskazini imepitisha style moja tu
ya nywele inayopaswa kufuatwa na wanaume wote ambayo ndio inayopendwa na
kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-Un.
Hapo
kabla wanaume wa nchi hiyo walikuwa wanaruhusiwa kuchagua kati ya style
10 za kunyoa zilizokuwa zimepitishwa, lakini sasa ni style moja tu
iliyopitishwa, huku wanawake wakiwa wamepewa style 18 za nywele.