BREAKING NEWS: BASI LA JAPANESE EXPRESS LATUMBUKIA MTONI WILAYANI MAKETE

Habari zilizotufikia katika chumba chetu cha habari cha eddy blog usiku huu, ni kwamba basi la kampuni ya Japanese Express linalofanya safari zake kati ya Makete - Njombe, limetumbukia kwenye mto eneo la Lwamadovela wilayani Makete

Basi hilo lilikuwa likitokea Njombe kuja Makete na ajali hiyo imetokea majira ya saa 11 jioni kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo

Wapo baadhi ya abiria waliojeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya Ikonda Consolata

Taarifa kamili ya ajali hiyo pamoja na picha zitakujia baada ya kikosi kazi cha Eddy Blog kufika eneo hilo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo