Mgeni
Rasmi Daniel Kadinde akimkabidhi zawadi mwanafunzi Monalisa Sungwa
aliyefanya vizuri katika masomo yake. Monalisa ni mmoja ya wanafunzi
anayesomeshwa na Compassion.
Mgeni rasmi Daniel Kadinde akizungumza na watoto wahitaji katika ukumbi wa kanisa la Anglikana Ipogoro katika siku ya shukrani.
baadhi ya watoto wenye uhitaji wakifatilia kwa makini burudani iliyokuwa ikitolewa na kwaya ya watoto wenzao wa Ebeneza.
Kwaya
ya watoto Ebeneza akitumbuiza katika siku ya kutoa shukrani kwa watoto
wenye uhitaji iliyofanyika katika ukumbi wa Kanisa la Anglikana Ipogoro.
Mwanafunzi bora Monalisa Sungwa akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake wanaosomeshwa na Compassion
========= ======= =========
Na Denis Mlowe,Iringa
JUMLA
ya watoto wahitaji 287 wamefaidika na ufadhili wa masomo ya elimu ya
shule ya msingi na sekondari unaotolewa na Kituo cha Huduma ya Mtoto cha
Anglikana Ipogoro kwa ufadhili wa shirika la Compassion.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa kituo hicho Kaini Mwakisyala wakati akiongea
na mwandishi wa habari hizi wakati wa siku ya Shukrani kwa Watoto
wahitaji uliofanyika katika kanisa la Anglikana tawi la Ipogoro mwanzoni
mwa wiki.
Mwakasyala
alisema kuwa watoto walionufaika na ufadhili huo ni kutoka mikoa sehemu
za Ilula, Ipogoro na maeneo jirani ya wilaya ya Kilolo huku wengi wao
wakiwa ni watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu kwani moja ya
malengo ya Taasisi hiyo ni kuwasaidia watoto wenye mahitaji hasa wa
kike ili waweze kupata elimu sawa na watoto wengine walio na wazazi.
“Watoto
hawa wako katika shule za Bweni hii ni kuwafanya waweze kupata huduma
zote muhimu ambazo ni chakula, malazi na muda wa kujisomea kwani watoto
wengi wa kike wakisoma shule za kutwa wanatumia muda mwingi kufanya
kazi za nyumbani na hivyo kukosa muda wa kujisomea na kucheza michezo
mbalimbali” alisema Mwakasyala.
Alisema
kuna umuhimu wa watoto wa wa jinsia zote kupa elimu itakayomsaidia
katika maisha yake ya kila siku na shirika hilo linamsomesha mtoto hadi
anapofikia elimu ya chuo na baada ya hapo atakuwa na uwezo wa
kujiendeshea maisha yake.
Mwakasyala
alisema watoto wa kituo hicho licha ya elimu ya kawaida wanapa elimu ya
ufundi wa kushona nguo, kufyatua matofali na ufundi mwingine unaoweza
kuwakomboa mara wamalizapo elimu zao na elimu hiyo hutolewa kutokana na
vipaji walivyonavyo.
Aidha
aliwataka wazazi kuwapa ushirikiano katika kuwaleta watoto waweze kupata
elimu stahiki kwa kugharamiwa kila kitu na shirika hilo zikiwemo ada,
sare za shule na vitabu mbalimbali vya kujisomea.
Mwakasyala
alibainisha changamoto wanazokumbana nazo mojawapo ni wazazi wengi
kushindwa kuwaleta watoto wao kwa misingi ya dini wakidhani kwamba
wakiwapeleka katika kituo hicho watabadilishwa dini walizozaliwa nazo
kutokana na chuo kumilikiwa na kanisa la Anglikana.
Kwa
upande wao watoto wa kituo hicho wakiwakilishwa na Monalisa Sungwa wa
kituo hicho alitoa shukrani kwa uongozi wa kituo hicho kwa kusimamia
huduma zote kwa watoto hao kwa ufanisi wa hali ya juu na kuwakomboa
katika kupata elimu iliyobora.
Sungwa
aliitaka jamii kuwashirikisha katika maswala ya kijamii kwa ngazi ya
kiwilaya katika kutoa maoni kutokana na mtoto kuwa na haki katika kutoa
maoni kwa jamii inayomzunguka.
“
Tumekuwa hatupewi fursa nyingi za kushiriki katika mafunzo na matamasha
pamoja na shughuli zingine za kijamii hakika hii inasababisha ushiriki
mdogo katika masuala ya kijamii naomba sana tushirikishwe katika kutoa
maoni” alisema Sungwa
Aidha
alisema wanakumbana na changamoto ya wazazi kutokuwa na ushirikiano na
kituo hasa pale wanapohitajika kushirikiana katika kuwafatilia watoto
maswala ya shuleni na tabia za watoto kwa ujumla.