Jeshi
la polisi mkoani Simiyu linawashikilia watu tisa wakiwemo wanawake
wawili wa kijiji cha Mwabulimbu wilayani Maswa kwa tuhuma za mauaji ya
kikatili ya kina mama wawili kuuawa na kuchomwa moto kwa kudaiwa kuzuia
mvua kunyesha.
Mbali na wanawake hao polisi pia inawashikilia viongozi wakuu wa jeshi la ulinzi wa jadi “Sungusungu” akiwemo Mtemi na Kamanda wake mkuu kwa tuhuma za mauji hayo ya kikatili kwa akina mama hao ambao baada ya kushambuliwa sehemu mbalimbali za miili yao walichomwa moto kwa madai ya kuzuia mvua kunyesha katika kijiji cha Mwabulimbu wilayani hapa.

Kamanda
wa polisi wa mkoa wa Simiyu Charles Mkumbo akiongea na waandishi wa
habari jana ofisini kwake alisema kuwa viongozi waliokamatwa ni Mtemi
mkuu wa sungusungu Ntalage Mabula (50) na Kamanda wake mkuu Sosoma
Mamuda (50) wote wakazi wa kijiji cha Mwabulimbu,kata ya Mwang’honoli
tarafa ya Sengerema wilayani Maswa mkoani hapa.
Wanawake
waliokamatwa kuhusiana na mauaji hayo ni Tabu Mongo (31) na Joyce Kija
(30) watuhumiwa wote ni wakazi wa kijiji cha Mwabulimbu kata ya
Mwang’honoli tarafa ya Sengerema wilayani Maswa.
Akielelezea
tukio hilo kamanda wa polisi alisema watuhumiwa wote walikamatwa
februari 4 kufuatia viongozi hao wakuu wa sungusungu mnamo februari pili
mwaka huu,kutoa amri na agizo la kupiga yowe na filimbi za hatari na
kukusanya wananchi waliowapiga na kuwaua na kuwachoma moto wanawake hao
wawili pia wakazi wa kijiji hicho.
Kamanda Mkumbo alisema kuwa kabla ya mauaji hayo, kijiji hicho na
maeneo mengine wilayani Maswa na hata mkoa wa Simiyu yalikuwa
yakikabiliwa na ukame wa mvua kutonyesha, na inadaiwa kuwa akina mama
hao waliomba kuchangiwa gunia moja kila mmoja kwa vile wanatoka katika
ukoo wa kichifu ili mvua iweze kunyesha.
Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo Mtemi wa sungusungu kwa kushirikiana na Kamanda wake mkuu wa Sunsungu Sosoma Mamuda (50) pia mkazi wa Mwabulimbu walipiga yowe na filimbi za hatari kuhoji kulikoni akina mama hao kuzuia mvua isinyesha kijijini hapo na ndipo walipoanza kuwaadhibu kwa kuwashambulia kwa silaha za jadi.
Kamanda Mkumbo alieleza kuwa watuhumiwa wote hao watafikishwa mahakani mara baada ya upelelezi kumalizika.