Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
HABARI kutoka Zanzibar zinasema uchaguzi mdogo wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki kisiwani humo unaendelea vizuri na wapiga kura wengi wamejitokeza kwenda kutimiza haki yao ya kimsingi.
HABARI kutoka Zanzibar zinasema uchaguzi mdogo wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki kisiwani humo unaendelea vizuri na wapiga kura wengi wamejitokeza kwenda kutimiza haki yao ya kimsingi.
Ulinzi umeimarishwa katika vituo vya kupigia kura.
Mwandishi wetu wa huko anasema jana kulikuwa na malumbano ya hapa na
pale kwa wanachama wa vyama viwili vikubwa vya siasa, Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Wananchi (CUF), kwani walikuwa
wakitambiana kila upande ukidai utashinda katika kinyang’anyiro cha leo.
Tutakuwa tukiendelea kuwapasha yanayotokea.