Baadhi ya watalii wakiwa eneo la hifadhi ya Gombe.
Na Ojuku Abraham
WABUNGE ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, wamekunwa na kitendo cha Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) kupitia hifadhi yake ya Gombe mkoani Kigoma, kujenga vyumba vinne vya madarasa ya Shule ya Sekondari ya Kagongo.

Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Mheshimiwa Abdulkarim Shah alitoa
pongezi hizo hivi karibuni kufuatia ziara yao katika hifadhi hizo za
taifa zilizo pembezoni mwa Ziwa Tanganyika.
Akizungumza kutoka mkoani Kigoma kwa njia ya mtandao, Meneja
Mawasiliano wa TANAPA, Pascal Shelutete, alisema Kamati hiyo ilitembelea
hifadhi hiyo na kujionea vivutio vingi vya utalii, ambavyo endapo
vitasimamiwa na kuendelezwa, vinaweza kuchangia ongezeko la pato la
taifa.
Wajumbe hao waliopokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi
walitembelea sehemu mbalimbali ikiwemo msitu mnene uliopo ndani ya
hifadhi hiyo pamoja na maporomoko ya maji ya Kakombe.