Mabao matatu ya Amisi Tambwe na moja la Jonas Mkude yamewafanya wekundu
wa Msimbazi waondoke na pointi zote tatu uwanja wa taifa dhidi ya JKT
Oljoro.
Ramadhan Singano "Messi" amezidi kuthibitisha ubora wote kwa
kupika mabao matatu mchezo wa leo. Jonas Mkude alikuwa wa kwanza kuliona
lango la JKT oljoro kufuatia kona ilivyochongwa na Ramadhan Singano,
huku dakika ya 24 Amisi Tambwe akifunga kufuatia pande la Singano.
Dakika ya 28 Tambwe aliziona nyavu za Oljoro
kufuatia mpira wa kutanguliziwa toka kwa Singano na kufanya hadi
mapumziko Simba waongoze 3-0.
Kipindi cha pili Amisi Tambwe
alijihakikishia kuondoka na mpira uwanjani kufuatia krosi ya Awadh Juma.
Simba sasa inatimiza pointi 30 ikiwa ni moja nyuma ya Mbeya City ambao
wanashikilia nafasi ya tatu wakiwa na pointi 31.
Matokeo mengine ni:
Ashanti United 0-2 Mgambo Shooting
Matokeo mengine ni:
Ashanti United 0-2 Mgambo Shooting