MSANII WA BONGO MOVIE MAARUFU KWA JINA LA TITO APATA AJALI MBAYA, TAZAMA PICHA HAPA

'Tito Zimbwe' Actor Bongo Movie's Tanzania

MSANII huyu maarufu na mkongwe katika tasnia ya filamu hapa nchini ambaye wengi walianzia kumtambua pale Kaole katika Tamthilia zilizotikisa Tanzania na vitongoji vyake,

Leo amepigiwa simu na mwandishi wa Blog hii baada ya kupata tetesi kwamba alipata ajali ya pikipi. 

Nguli huyo wa filamu alifunguka kuwa ajali hiyo ilitokea mnamo siku ya Ijumaa 7/FEB/2014 usiku majira ya saa tano na nusu,
Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni tuta lililowekwa barabarani bila alama yeyote au kiashiria cha kuonyesha kuwa eneo hilo kuna tuta kwahio dereva upunguze mwendo.

Alikuwa akitokea kigogo sambusa kuelekea kinondoni kufika maeneo ya kigogo lutihinda mkabala na Shule ya Msingi Lutihinda Primary School alishangaa ghafla amedunda kwenye tuta na kupaa hewani kutua chini akashindwa kuizuia pikipiki ikamgaragaza kwa bahati nzuri mungu mkubwa kwakweli aliumia lakini hakuvunjika popote zaidi ya kuchubuka mikononi na miguuni.

Maranyingi msanii huyo hutumia gari lakini sikuhio aliamua kutoka na pikipiki kumfuata rafiki yake mpendwa Beni Branco mzee wa Vituko Vituko aliyekuwa swaiba sana wa marehemu Steven Kanumba, Ajali hiyo ikawa mwisho wa safari ya kwenda kumsalimu Beni Branco.

Mpaka sasa 'Tito Zimbweyupo Kinondoni katika Hospitali ya Private ya Doctor Mvungi. Anaendelea na matibabu, Hali yake ni nzuri kwa mujibu wa yeye mwenyewe huwenda akaruhusiwa kesho asubuhi m/mungu akipenda.

Shemejietu (Mkewe) kushoto akimliwaza kaka Tito Zimbwe
usijali shemeji mzee atapona sisi ndugu zake yani masainyotambofu.com kwa ujumla tunamuombea kwa pamoja huku Anko Beny akiendelea kumpa Vituko vya nguvu...

 
Hali ya mgonjwa kidogo inaridhisha..! Ha ha haaa.. Mpaka anatasabamu?''
 
HUYO hapo kulia ndio Beny Branco rafiki yake Tito Zimbwe na wa katikati ni Director Faridu uwezo kushoto anaepewa glass ya naniliu ni mgonjwa mwenyewe..!
 Du! Beny ana visa! Hadi Hospitali?.. Beny umepinda Chaliangu... We ni kwere arifff...


PICHA kwa hisani ya Website ya masainyotambofu.com


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo